Horror
FLORINE WILHELM SENGA
2
2000
UTANGULIZI: ADHABU YA KAFIRI
Wanasema uzuri ni zawadi, lakini kwa wengine ni laana inayoficha mashimo ya kuzimu. Zawadi ya uumbaji inageuka kuwa mlango wa maangamizi kwa binti huyu, aliyependelewa kwa uso wa malkia na shepu ya mantashau.
Tangu akiwa kigori, macho ya wanaume yalimuandama kama kivuli chake mwenyewe, na maneno ya vishawishi yakawa mlo wake wa kila siku. Polepole, moyo wake ulianza kujifunza utamu wa uzinzi kabla haujajua thamani ya heshima. Hapo ndipo pepo la tamaa lilipoanza kumvuta taratibu, kama upepo wa mchana unaoleta dhoruba ya usiku.
Lakini kilichoanza kama raha, kinageuka kuwa kifungo kisichoonekana. Baada ya kuingia kwenye kitanda cha mume wa chifu wa kabila lao, binti huyu anafungua rasmi mlango wa kuzimu.
Malkia Katei, mwanamke mwenye nguvu za ajabu za giza, aliyetambua usaliti huo hakumwacha salama. Kwa hasira na kisasi, alimrushia laana ya kipepo chenye kiu ya ngono isiyoisha, kiu ya uharibifu.
Sasa, akiwa chini ya ushawishi wa nguvu hizo chafu, binti huyu anaota, anatamani, na anapanga jambo la kutisha; kulala na baba yake mzazi. Ni mzimu gani unamsukuma? Ni tamaa au laana? Je, ataweza kuvuka mstari huo wa mwisho wa ubinadamu? Na kama ataweza, dunia yake itageukaje?
Adhabu ya Kafiri sio simulizi ya kawaida. Ni hadithi ya tamaa isiyo na mipaka, laana ya uzuri, na maangamizi ya nafsi. Hapa utashuhudia vita vya mwili, roho, na damu...kwani kuna laana zisizovunjika kwa sala tu, bali kwa damu na majuto ya daima.