Fantasy
FLORINE WILHELM SENGA
0
2000
MUHTASARI WA RIWAYA: NABII JONATHAN – Wakili wa Kifo
Mwandishi: Florine Willy
Mchungaji wa kawaida anageuka kuwa nabii mwenye jina kubwa; sio kwa miujiza ya uponyaji, bali kwa kipawa cha kutisha: kutabiri vifo vya watu ndani ya siku tatu hadi tano. Na kinachotisha zaidi… wale anaowatabiria, hufa kweli!
Umaarufu wa Nabii Jonathan unapaa, watu wakimiminika kutoka kila kona kutafuta ulinzi dhidi ya kifo kilichotabiriwa. Lakini anawapa habari njema waumini hao, ya kwamba Bwana amesikia kilio chao. Walio tayari kutoa maisha yao sadaka wanabaki hai. Wanaokataa, wanaangamia kwa kifo cha ghafla, ajali za kutisha, au maradhi ya ghafla.
Mariam Mwandu—mwandishi wa habari jasiri anakuwa mtu wa kwanza kutilia mashaka mfuatanao wa matukio hayo. Anapoamua kufuatilia kwa karibu vifo hivyo, ghafla maisha yake yanakuwa hatarani kuliko wakati mwingine wowote ule.
Je, ni kweli Nabii Jonathan anasikia sauti ya Mungu—au ni mjumbe wa mauti anayejificha nyuma ya collar takatifu?
Nabii Jonathan – Wakili wa Kifo. Uhai wako unaweza kuwa sadaka yake inayofuata...