MSAMAHA VS KISASA; Sanaa Zinazokinzana

Non- Fiction

FLORINE WILHELM SENGA

0

2000

UTANGULIZI

Msamaha ni nini hasa?
Ni kuachilia makosa, maumivu, na dhuluma bila kulipiza. Lakini je, hilo linawezekana kila wakati?

Kisasi ni nini basi?
Ni jibu kali kwa maumivu lenye kulipiza kwa lengo la kufidia, kuonesha hasira au kuleta usawa. Lakini je, kisasi hutuliza roho au huongeza maumivu?

Kwa nini mtu huchagua kisasi badala ya msamaha?
Kwa sababu ya hasira, tamaa ya haki, au maumivu ya kudharauliwa. Wengine husema, “Samahani ni udhaifu, kisasi ni ujasiri.”

Kuna aina ngapi za kisasi?
Je, ni lazima kisasi kiwe cha damu? Au maneno, kupuuza, au kimya kingi kinaweza kuwa kisasi? Hebu tutafakari.

Kuna faida yoyote ya kulipiza kisasi?
Ndiyo au la? Wengine hudai huleta nafuu ya muda, lakini ni nafuu au ni sumu tamu?

Msamaha je? Unasaidia kweli?
Ndiyo. Unatibu roho, unafungua milango ya amani ya ndani. Lakini… unajua kwamba kuna walioathirika zaidi kwa kusamehe?

Kuna aina ngapi za msamaha?
Kuna wa ndani kwa ndani, wa kijamii, wa kimya, na wa wazi. Je, unajua msamaha unaweza kuwa silaha kubwa kuliko kisasi?

Faida za msamaha ziko wazi. Vipi kuhusu hasara zake?
Kusamehe bila mipaka kunaweza kukufanya udharaulike, kushambuliwa tena, au kujikuta unakiangamia ndani kwa ndani. Unacharoje mpaka wa rehema?

Je, kuna mtu aliyesamehe na kuangamia?
Ndiyo. Na kuna aliyelipiza kisasi na kuangamia pia. Huu ni mchezo unaohitaji umakini wa nafsi na roho; sanaa ya kuchagua barabara ya nuru au giza.

Sasa swali ni hili:
Ukilazimika kuchagua leo ; ungechagua msamaha au kisasi? Njia bora zaidi ni kujifunza kutoka kwa waliopita mbele yako: waliolipiza, waliokosea, walioteseka, na waliosamehe.

Twende safari hii pamoja, sako kwa bako. Tutachambua kila hoja, tutaingia ndani ya nafsi za wanadamu, tutatumia mifano ya kweli, na mwishowe, utatoa hukumu yako mwenyewe.
Je, utaelekea upande wa msamaha au utachagua kisasi?

Karibuni katika udadavuzi wa kina, tuzichambue sanaa hizi kongwe zinazokinzana.