Fantasy
FLORINE WILHELM SENGA
7
2000
Usipochafuka utajifunzaje? Wakati mwingine, kukosea na kushindwa, aibu na fedheha ni njia ya kujitengenezea kesho bora zaidi. Ni kuandaa mlango wa kutufikisha kwenye nchi ya ahadi. Dhahabu shurti ipitishwe katika moto ili iwe bora.
Katika utoto na hekaheka za ujana, kuna fedheha nyingi zilizonipata. Wakati mwingine nikihatarisha si tu heshima bali hata usalama wangu. Mwisho wa yote, nikajifunza upya kuyaishi maneno ya Baba Gombera, Mwalimu na kiongozi wangu wa kiroho pale Kaengesa Seminary, Padre Joachim Kalumanzila Sangu;
"Fanya jambo sahihi, kwa muda sahihi na mahali sahihi..huu ndiyo msingi wa muda wote wa nidhamu thabiti."
Mara nyingi alisisitiza kwa lugha ya kingereza, "Do the right thing, at the right time and the right place...unless you will suffer the consequence!"
Ndani ya kitabu hiki nimekuandalia visa na mikasa katika mtindo wa kuburudisha na kuelimisha, kwa namna itakayokuachia kicheko na kumbukumbu zisizosahaulika.
Nakukaribisha katika mtiririko wa fedheha zilizonifunza nidhamu.