NGUVA (Jazanda La Kuzimu)

Fantasy

FLORINE WILHELM SENGA

0

2000

Veronika, mwanadada msomi na mrembo, wakili msomi katika kampuni kubwa ya kisheria; anakutana na mteja wa aina. Ni mwanaume kijana, mtulivu, mwenye kunuka fedha; aliyekuja kuomba huduma za kisheria.

Akili zinamruka, hisia zinatekwa. Wajihi na hulka yake vinammaliza kabisa Veronika. Katika kazi yake, amekuwa akikutana na wanaume wa kila aina na wote walikuwa na tabia za kufanana. Huyu mwanaume hafanani na yeyote kati ya wanaume hao, tofauti inayomfanya amhusudu ghafla. 

Siku aliyopanga kwenda kutembelea kampuni ya kijana huyu, ndiyo siku alipofunguliwa mlango wa kuzimu. Safari iliyoanza kwa mwanga wa matumaini ya huba jipya, inaishia katika gazi la ngome isiyofahamika; chini ya kiumbe hatari kilichopewa jina la Nguva....Ni wapi huko? Atapataje kupona?