NILIWAHI KUWA PADRE

Thriller

FLORINE WILHELM SENGA

0

2000

Ndani ya kuta za gereza, yumo mfungwa mwenye umri wa miaka 56 aliyehukumiwa kifungo cha maisha. Ni kati ya wafungwa wachache ambao hawakuwahi kutembelewa na ndugu, jamaa au rafiki. 

Katikati ya msimu wa mmoja wa masika, kwa mara ya kwanza ndani ya miaka saba aliyotumikia kifungo chake, mfungwa huyu anatembelewa na mwanamke mwenye ulemavu. Sura yake inaonesha uchovu wa safari na madhila mazito ya maisha. 

Mara baada ya kumtambua mwanamke huyu, mfungwa huyu anaangua kilio cha kushtua. 

Huyu mwanamke mlemavu ni nani? Na huyu mfungwa ni nani?