Thriller
FLORINE WILHELM SENGA
9
2000
UTANGULIZI
Kuna msemo wa kale usemao, "mke wa mtu ni sumu." Lakini ikiwa sumu hiyo haina madhara hata kwa mende, basi itamtisha nani?
Brian hakujali maonyo wala kufanya tahadhari juu ya hatari inayoweza kumpata. Akiwa mateka wa tamaa zake, anafanikiwa kutimiza azma ya kulala na mke wa Amani,mwanaume mpole ambaye tayari alikuwa amempa angalizo kuhusu mwanamke huyo. Lakini raha ya kitendo hicho ni ya muda mfupi mno, na badala yake inageuka jinamizi litakalomburuza katika giza kuu la mateso ya nafsi.
Baada ya tukio hili, Amani anapotea ghafla na bila maelezo yoyote. Ameacha nyuma fumbo kubwa linalomtesa Brian, na sasa jamii nzima inamtambua Brian kwa jina lenye utata: Mume wa Wajane.
Lakini kwanini aitwe hivyo? Je, kuna siri gani nyuma ya pazia hili la kiza? Je, Amani yu hai ama ameshaondoka duniani? Na je, hukumu aliyopaswa kuogopa Brian sasa ndiyo imeanza kumtafuna taratibu?
Fuatilia simulizi hii yenye msisimko na fumbo zito, ujionee jinsi Brian anavyosakamwa na kivuli cha dhambi yake huku ukweli ukizidi kuwa mgumu kuliko dhana yenyewe.